King Kiba apokea tuzo hii ya heshima

69

Kiba2

Hitmaker wa Mvumo wa Radi Ali Kiba amekabidhiwa tuzo ya heshima ya Plaque iitwayo “Nyota wa Mchezo” kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM.

Mkali huyo ametunukiwa tuzo hiyo kutokana na jitihada zake katika tasnia ya muziki kwa kupeperusha bendera ya Tanzania na kuwahamasisha wasanii chipukizi kuwepo katika game la muziki.

Kiba anawafuata wenzake wawili waliopewa awali ambao ni Vanessa Mdee aliyekabidhiwa mwezi Januari mwaka huu na Diamond mwezi wa tatu.

Video yake ya mpya ya Mvumo wa Radi imeshafikisha viewers millioni 1.1 kupitia YouTube ambapo ilitambulisha kinywaji chake kipya cha Mofaya Energy Drink.