Maandamano yapamba moto Gaza

77

maandamano palestina

 

Maandamano mapya dhidi ya Israel yanatarajiwa kufanyika huko Palestina leo, siku moja baada ya wanajeshi kuwaua watu 58 huko ukanda wa Gaza.

Jumatatu ilikuwa siku mbaya zaidi tangu maandamano kuanza kwenye mpaka wa Gaza wiki saba zilizopita. Leo itakuwa ni maadhimisho ya miaka 70 ambayo Wapalestina wanayataja kama Nakba – ambayo ni maadhimisho ya kuhamishwa kwa Wapalestina kufuatia vita vya kuundwa kwa Israel.

Msukosuko mpya unatarajiwa huko Gaza siku ambayo yatafanyika maziko ya wale waliouawa.

Ghasia za jana Jumatatu zilizuka wakati ambapo Marekani ilikuwa inafungua ubalozi wake huko Jerusalem hatua iliyowakasirisha wapalestina. Wapalestina wanadai Yerusalem Mashariki ni mji mkuu wa taifa la baadaye la Palestina na kuitaja hatua ya Marekani kama inayounga mkono Israel kuweza kudhibiti mji huo wote inaoutaja kuwa mji wake mkuu.

Maafisa wa Palestina wanasema takriban watu 2,700 walijeruhiwa wakati wa ghasia hizo siku ya Jumatatu, na ghasia hizo zimekuwa ni ghasia zilizo mbaya zaidi kuwai kushuhudiwa huko Gaza tangu mwaka 2014.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema jeshi lake lilikuwa linajilinda dhidi ya watawala wa Gaza, Hamas ambao anasema lengo lako ni kuiangamiza Israel. Wapalestina walikuwa wanaandamana siku ya Jumatatua jinsi wamekuwa wakiandana kwa wiki sita katika sehemu ya maandamano yaliyochochewa na Hamas yanaofahamika kama “Great March of Return”.

Hata hivyo yale ya Jumatatua na leo Jumanne yanakwenda sambamba na maadhimisho ya kuundwa taifa la Isreal mwaka 1948 na kuhama maelfu ya wapalestina kutokana na vita vilivyofuatia.

Chanzo: BBC Swahili (http://www.bbc.com/swahili)