Mke wa Trump afanyiwa Upasuaji

73

melania trump

Mke wa Rais wa Taifa la Marekani, Bibie Melania Trump amefanyiwa upasuaji wa figo. Ofisi yake ilisema kuwa madaktari walifanya upasuaji huo kwenye hospitali ya Walter Reed National Military Medical Center.

Upasuji huo ulikuwa wenye mafaninikio na hakukuwa na matatizo yoyote kwa mujibu wa msemaji wake. Bi Trump, mwenye miaka 48, anatarajiwa kutumia muda mwingi wiki hii kupata nafuu hospitalini huko Bethesda, Maryland.

Rais Trump aliandika katika Twitter kuwa alikuwa njiani kwenda kumtembelea hospitalini.

Wiki iliyopita Bi. Trump alizindua mpango kwa jina “Be Best” wenye lengo la kuwafunza watoto kuhusu masuala ya kijamii, afya kuhusu hisia na kimwili.

Alisema kampeni hiyo ina lengo la kuhakikisha maisha yenye afya na kuzuia dhuluma.
Pia ilitangazwa Jumatatu kuwa aliyekuwa kiongozi wa wengi wa seneti wa chama cha Democratic,Bw. Harry Reid, 78, alikuwa amefanyiwa upasuaji wa kongosho.

Familia ya Bw Reid ilisema madaktari kwenye hospitali ya Johns Hopkins Hospital huko Baltimore walikuwa na uhakika kuwa upasuaji huo ulikuwa wenye mafanikio na anapata nafuu vizuri.
Madaktari walikuwa wamegundua tatizo mapema wakati wa uchunguzi wa kawaida wa kiafaya, kwa mujibu wa taaarifa.

Seneta wa Republican John MacCain ambaye mwenyewe anaugua saratani ya ubongo ni kati ya wale waliomtumia ujumbe wa heri njema.

Chanzo: BBC Swahili(http://www.bbc.com/swahili)