Hivi Punde: Lulu atoka Gerezani

288

Lulu4

Muigizaji maarufu wa Tasnia ya Filamu Tanzania, Bibie Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu aliyehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba 13 mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, amebadilishiwa adhabu na Mahakama na sasa atafungwa Kifungo cha nje yaani “Community Service”.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

“Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi. Hii si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, kitaalamu tunaita ‘community service’” amesema Mboje.

Kesi ya Lulu ilikuwa ikisikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Ikiongozwa na Jaji Sam Rumanyika. Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mbonje amethibitisha kuwa jumamosi, Mei 12, 2018 msanii wa maigizo nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu aliachiwa huru na Mahakama kuu ya Tanzania mara baada ya kubadilishiwa kifungo na kutumikia kifungo cha nje.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba 13 mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Chanzo: Global Publishers ( http://www.globalpublishers.co.tz )