Kesi ya Mbowe na wenzake kuunguruma leo Kisutu

92

MBOWE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeanza kusikiliza kesi dhidi ya Mbowe na viongozi wenzake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ambapo wanakabiliwa na mashitaka ya kufanya mikusanyiko isiyo halali.

Viongozi wa chama hicho waliofika mahakamani hapo akiwemo Mbowe, ni Peter Msigwa, Salum Mwalimu, John Mnyika, Esther Matiko, Dk. Vicent Mashinji.

Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya hawakufika mahakamani hapo kutokana na kilichoelezwa na wakili wao, Peter Kibatala, kuwa ni matatizo ya usafiri.