Makala: Maisha na Kifo cha Hayati Edward Sokoine

118

Watu wakiulizwa Kiongozi gani Tanzania ukiacha Nyerere ungependa mfano wake uigwe? Wengi husema Sokoine. Chuo cha Kilimo cha Morogoro kinaitwa Jina lake yaani Sokoine University of Agriculture (SUA). Je, huyu Sokoine ni nani?.

moringe

Hayati Edward Moringe Sokoine, alizaliwa tarehe 1 Agosti 1938, alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kuanzia tarehe 13 Februari 1977 hadi tarehe 7 Novemba 1980 tena akawa Waziri mkuu toka tarehe 24 February hadi tarehe 12 Aprili 1984.  Alizaliwa Monduli Mkoani Arusha Tanzania, alipata elimu ya msingi na sekondari katika miji ya Monduli na Umbwe toka mwaka 1948 hadi 1958. Mwaka 1961 alijiunga na chama cha TANU baada ya kuchukua masomo katika Uongozi nchini Ujerumani 1962 hadi mwaka 1963. Aliporudi kutoka Ujerumani alikuwa Afisa Mtendaji wa Wilaya ya Masai, tena akachaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Masai. Mwaka 1967 alikuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Usafiri na Kazi.

Mwaka 1972 alikuwa Waziri wa Usalama. Mwaka 1975 alichaguliwa kwenye Ubunge tena wakati huu kupitia Monduli. Miaka miwili baadae akawa mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha  Mapinduzi (CCM), 1977 alianza muhula wa kwanza ofisini akiwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania. Muhula huu ulidumu hadi 1981, baada ya kutulia kwa kipindi cha mwaka akawa tena Waziri Mkuu mwaka 1983, alikaa mwaka mmoja ofisini mpaka alipofariki Aprili 1984 kwa ajali ya gari.

Sokoine Car

NYERERE ANATANGAZA KIFO CHA SOKOINE, NCHI INAZIZIMA, WATU WANAZIMIA KWA SIMANZI. 

Ilikuwa majira ya jioni tarehe 12 April 1984 kwenye taarifa ya habari ya saa 10.00 jioni mwaka 1984; kama ilivyokuwa kawaida ya nchi zote za Kikomunist vyombo vya habari vyote vilikuwa ni mali ya serikali, na ilikuwa na desturi ya kila Mtanzania kuhakikisha anakuwa karibu na redio kila inapofika wakati wa taarifa za habari kwa vile ilikuwa ndiyo njia pekee ya kupata habari mbali mbali za ndani na nje ya nchi. Ilikuwa ni desturi ya Watanzania popote walipokuwa na wakati wowote inapofika muda wa taarifa ya habari shughuli zote husimama kwa muda wa dakika 10 ili kila mtu asikilize mambo muhimu yaliyotokea ndani na nje ya nchi.

Nyerere akimlilia Sokoine

Katika taarifa ya habari ya saa 10 jioni ya siku hiyo ilikuwa tofauti na taarifa za habari za siku nyingine kwa vile siku hiyo mtangazaji wa taarifa ya habari alikuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na alianza kwa kusema:
“Watanzania wenzangu, ndugu yetu, kijana wetu, Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine amefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea huko Dakawa nje kidogo ya mji wa Morogoro akitokea Dodoma kulihutubia bunge; ajali hiyo ilitokea wakati alipokuwa katika ziara yake ya kukagua mashamba ya mahindi katika mkoa wa Dodoma na Morogoro. Msafara wa waziri mkuu ulivamiwa na gari aina ya Toyota Land Cruser ya mkimbizi mmoja wa kutoka Afrika ya Kusini kwa jina la Dube ambaye alikuwa anaishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Mzimbo mjini Morogoro; Dube alisimamishwa na polisi lakini alikaidi na kwa vile alikuwa katika mwendo mkali akasababisha ajali kwa kuigonga gari aina ya Mercedes Benz iliyokuwa imembeba waziri mkuu na kusababisha kifo chake.
Watanzania wenzangu nawaombeni sana mkubali kwamba Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine amefariki kwa ajali ya gari.”

Hayo yalikuwa ni maneno yaliyotamkwa na Mwalimu Nyerere katika taarifa ya habari, alipokuwa anatoa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine. Ukitaka kuthibisha maneno haya Nyerere waweza kuyapata kwenye maktaba ya redio Tanzania, au unaweza pia kuyakuta kwenye maktaba za magazeti ya Uhuru na Daily News.

Baraza la Mawaziri akiwepo marehem Sokoine wa nne kutoka kushoto mbele.
Baraza la Mawaziri akiwepo marehem Sokoine wa nne kutoka kushoto mbele.

Wengi wamesema alikuwa ni mtu aliyepanda usawa kwa kila mtu, aliamini  kila mtu anaweza kuwa na maendeleo kama akijituma katika kilimo na sehemu alipo pamoja na kujitegemea akiwa ni wakala wa mabadiliko katika nchi, mtu asielaumu na mwaminifu.

Chanzo: Motive Media (http://www.motivemediatz.com/2015/04/leo-ni-kumbukumbu-ya-kifo-cha-edward.html )