Mhagama: Hatuhusiki na utozaji wowote wa fedha

69

Mhagama

Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama imedai serikali haihusiki kwa namna moja ama nyingine na Taasisi inayowatoza wanawake shillingi elfu kumi kupitia jina la Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan katika mkoa wa Kigoma.

Akitoa majawabu katika mkutano wa Bunge unaoendelea huko mjini Dodoma ambapo swali hilo linasema hivi kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kigoma, Josephine Gezebuke:

Katika Mkoa wa Kigoma iko NGO’s ambayo imezunguka kwa muda wa wiki mbili katika wilaya zote saba ikiwatoka wanawake sh. elfu 10, 10 na kuwapigisha picha na kuwaahidi kwamba serikali itatoa mikopo kwa kupitia mfuko wa Makamu wa Rais, Mama Samia, Je? ninataka serikali inieleze mpango huo wa kutoa pesa kupitia mfuko wa Mama Samia upo?

“Shughuli zote za uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi katika nchi yetu ya Tanzania zinasimamiwa na sera 2004 na sheria ya uwezeshaji wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 ambayo inaruhusu uanzishwaji wa Taasisi mbalimbali kisheria, Taarifa kuhusu Taasisi hiyo zilishapatikana ndani ya serikali na ofisi ya Makamu wa Rais ilishatoa tamko la kuikana taasisi hiyo kwamba haihusiki nayo”

“Ninaomba nichukue nafasi hii kuuagiza uongozi wa Mkoa wa Kigoma kuifuatilia taaisi hiyo na kuikana na kuipa maelekezo kwamba ofisi ya Makamu wa Rais aihusiki na jambo hilo na kama wanaendesha shughuli hizo kwa kutumia sheria taratibu nyingine wanapaswa kujieleza kwa kutumia sheria na taratibu zingine walizozifauta lakini sio ofisi wa Makamu wa Rais.”

Bi Jenista ameongeza kuwa endapo Taasisi hiyo itaendelea kufanya tabia hiyo ya udanganyifu kwa wananchi basi hawatasita kuchukua hatua kali.