TRA yakusanya Trilioni 11.78

83

Katika Kipindi cha miezi tisa ya Mwaka wa Fedha 2017/18 kuanzia Julai 2017 hadi Machi 2018, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya jumla ya Shilingi Trilioni 11.78 ikilinganishwa na Shilingi Trilioni 10.86 ambazo zilikusanywa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17. Kiasi hiki ni sawa na ukuaji wa asilimia 8.46.

Katika Mwezi wa tatu pekee TRA imekusanya jumla ya Shilingi Trilioni 1.54 ikilinganishwa na mkusanyo ya mwezi Machi 2017, ambapo ilikusanya Shilingi Trilioni 1. 34 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 14.49.

Tazama:

taarifa ya tra