Haroub: Huwezi kumdharau mpinzani, tunafahamu ni timu nzuri

118

Yanga

Beki na nahodha wa klabu ya Yanga SC Nadir Haroub “Cannavaro” ameeleza kuwa wako tayari kuikabili Rayon Sports katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika siku ya Jumatano Mei 16 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mahojiano hayo na waandishi wa habari, beki huyo amedai kuwa timu pinzani iko vizuri kwa hiyo huwezi kumdharau kwa kuwa na yeye amepambana hadi kufika hapo alipo.

“Huwezi kumdharau mpinzani,tunafahamu ni timu nzuri ndiyo maana wamefika hapo walio, tumejiandaa vizuri lengo letu ni kushinda mchezo ili tuweke nafasi nzuri kwenye kundi,muhimu ni mashabiki kujitokeza kwa wingi ili tushinde pamoja na tuchukue pointi tatu pamoja”

Yanga wanaelekea kwenye mechi hii wakiwa hawajapata ushindi ndani ya mechi saba mfululizo ukiongeza na ile mechi ya ufunguzi walipocheza dhidi ya USM Algiers walipochapwa 4-0.