Kane ampa dongo hili Salah

155

salah

Salah

Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspur Harry Kane amemkingia kifua mshambuliaji wa Liverpool, Mohammed Salah kuwa kama kweli anataka kujulikana kuwa ni mfungaji bora atwae kiatu hicho cha dhababu mara mbili mfululizo kama alivyofanya yeye.

Salah amemaliza msimu kwa mabao 32 baada ya kufunga moja wakati klabu yake ikiikung’uta Brighton goli 4-0 huku mwenzake akifanikiwa kufunga hatrick katika mchezo mkali ulioisha kwa bao 5-4 dhidi ya Leicester City na kufikisha magoli 30.

Harry-Kane-Football3651

Kane

Kane binafsi ameeleza ushindani ni jambo linalovutia hasa kwa ligi ya Uingereza na kunakuwa na msimu wachezaji wawili wanamaliza wakilingana magoli sawa.

“Ni vizuri kuwa na ushindani, na inavutia zaidi kuona kwenye ligi ya Uingereza kunakuwa na wachezaji wawili waliyofanikiwa kufunga mabao 30.

Binafsi yalikuwa ni malengo yangu kuona kipaji changu kinakuwa ukilinganisha na mwaka jana, wakati nilifunga mabao 29 msimu huu nimefikisha 30 kwangu naona vizuri.

Mo amefanya vizuri mwaka huu, hakika anastahili kupata tuzo hiyo ya kiatu cha dhahabu naangazia zaidi kwenye ushindani wetu mwaka ujao.

Kila mchezaji anahitaji kuwa na muendelezo mzuri kila msimu na hiyo ndiyo tafsiri ya mchezaji mzuri kuwa bora. Amefanya kitu kizuri na kinashangaza msimu huu na anaonekana kuwa mchezaji bora tutaona kama tutaendelea kuwa hivi msimu ujao.”

Hata hivyo mshambuliaji huyo amekuwa na furaha kutokana na kwamba alishawahi kunyakua kiatu hicho mara mbili kwa mpigo baada ya kufikisha magoli 25 na 29.