TFF yamuomba Magufuli kufanya jambo hili

103

Magufuli3

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Rais wake Wallace Karia umetuma maombi kwa Waziri mwenye dhamana ya michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amuombe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli awakabidhi taji mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba.

Wekundu wa Msimbazi watapewa kombe lao siku ya Jumamosi Mei 19, 2018 ambapo wanakipiga na Kagera Sugar katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo siku hiyo, Rais Magufuli atakabidhiwa kombe la CECAFA U17 Championship na timu ya vijana iliyochini ya miaka 17 Serengeti Boys baada ya kuibuka kidedea katika fainali iliyofanyika huko nchini Burundi.

Bwana Wallace amesema haya:
“Tumeandika barua kwa Waziri Mwakyembe amuombe ili Rais Magufuli akabidhiwe kombe la CECAFA U17 baada ya timu yetu kufanikiwa kushinda kombe hilo huko Burundi. Waziri amesema atajitahidi kwa kila njia ili Rais akubali”
“Pia kwa sababu siku hiyo Simba itakuwa inacheza mechi yake ya mwisho ya ligi kwenye uwanja wa nyumbani, tunafanya utaratibu Rais Magufuli awakabidhi kombe lao la ubingwa wa ligi kuu.”