Mfumuko wa bei ya vyakula nchini washuka

60

Mfumuko2

Mfumuko wa bei kwa vyakula nchini unaripotiwa kushuka kwa asilimia 0.2 ambapo awali ilikuwa kati ya asilimia 4.1 hadi asilimia 3.9.

Taarifa hiyo imetolewa na Taasisi ya taifa ya Takwimu kuwa pamoja na gharama za bidhaa za watumiaji, kupanda kwa asilimia 1.2, hiyo imekuwa na ufadhali ukilinganisha na rekodi ya mwezi Januari mpaka Februari mwaka huu.

Ongezeko hili limeegemea kwenye sekta ya chakula huku bidhaa hizo ni kama mchele ambapo ongezeko ni asilimia 3.8, mahindi (4.1%), samaki (2.6%), mboga za majani (5.3%) na unga wa muhogo (1.9).

Hii inasemekana kutokana na utumiaji mwingi wa mafuta ya taa, mkaa na diseli.

Kwa upande mwingine, mchumi Dr. Abel Kinyondo kutoka taasisi ya utafiti ya kupunguza umaskini ameeleza kuwa jambo kuu linalosababisha mfumuko kupanda zaidi ni chakula.

“Kitu kimoja kinachoathiri mfumuko wa bei ni chakula hata kama bidhaa nyingine zitashuka gharama bado mtumiaji hatahisi nafuu hiyo kwa kuwa matumizi yao makubwa yako kwenye chakula kwanza kabla ya sehemu nyingine”

Aliongeza:
“mfano unapozungumzia gharama za usafirishaji kutoka mashambani kupanda, moja kwa moja mlaji wa mwisho atapata bidhaa hizo kwa gharama ya juu”

Chanzo: BBC