Dogo Janja amuenzi mkewe kwa hili

73

janjaro

Tangu walipofunga ndoa yao Dogo Janja na Irene Uwoya imekuwa vigumu kuwakosa kwenye vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari nchini na kwa sasa Dogo Janja amekuja na suala la kuchora tattoo ya Irene Uwoya kwenye kwapa.

Kuchora tattoo inaweza isiwe tatizo kwani kila mtu anaweza kuchora ila suala ni eneo tattoo yenyewe imechorwa si ya kawaida.

janjar

Kupitia Instagram Dogo Janja ameweka picha hiyo na kuandika; I made this infinity Promise for you @ireneuwoya8 #NoMoreDramašŸŒ¹.

Aidha hatua hiyo imekuja baada ya Irene Uwoya kufanya kitu kama hicho miezi kadhaa iliyopitia ambapo Dogo Janja alimtaka kuchora nyingine.

janja

Dogo Janja na Irene Uwoya waliripotiwa kufunga ndoa November 25, 2017, hata hivyo ni vigumu kutaja tarehe kamili kutokana na namna walivyoliweka suala hilo hasa kwa upande wa vyombo vya habari na mitandao.