Harmonize abwatuka haya kwa Wolper

93

Harmonize

Hitmaker wa “DM Chick” Harmonize ametema cheche kuhusu mpenzi wake wa zamani Jacquiline Wolper baada ya kupost ujumbe Insta list ya wanaume ambao alishawahi kuwa na mahusiano nao.

Taarifa hizi zimetapakaa kutokana na kwamba Harmonize sasa ana mrembo mwingine aitwaye Sara hivyo akachukua nafasi hiyo ya kumpakazia mpenzi wake wa awali Wolper kupitia akaunti yake ya Insta kuwa ametembea na wanaume 12:

harmonize_tz….!!! zinaitwa hasira za fundi chereheni mchaga…..!! sasa jamani #sarah wawatu na huyu dada nani ni mlezi wa wana…..??? #Kikosi (A)
1 Dallas
2 mkongo
3 Simba
4 makochali
5 G modo
6 Chidi mapenzi
7 Konde_ boy
8 Chazi baba
9 brown
10 Engene
11 Jux, hebu nisaidie kuwatag kikosi (B) na (C) wacha niende zangu Mwanza.

Baada ya kuonekana akishambuliwa kupitia ujumbe huo, Harmonize akafuta haraka lakini muigizaji Shamsa Ford alikasirika baada ya kuona jina la mumewe Chid Mapenzi

“Harmonize nakuheshimu sana mdogo wangu wangu, please nisingependa kuona jina la mume wangu kwenye huo ujinga wenu, Chidi kwenu anaweza akawa mshikaji kwangu ni mume.Kulikuwa hakuna haja ya kuweka jina lake wakati unajua ana maisha mengine. Tushichukuliane poa,”

Harmonize2

Harmonize na Sarah

Hii inasemekana kwamba uhusiano wa Harmonize na Sarah imebamba sana wikiendi hii iliyopita huku taarifa nyingine zikiibuka kuwa mpenzi wa Harmonize anatembea na Bodyguard wa Chibu Dangote, Mwarabu Fighter.

Chanzo: Bongo 5