Hatimaye Abdul Nondo afikishwa Mahakamani

99

nondo

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amesafirishwa usiku wa kuamkia leo kwenda mkoani Iringa kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayomkabili.

Abdul Nondo amerudishwa mkoani Iringa na kufikishwa Mahakama ya Wilaya ambapo awali Nondo alitolewa Iringa baada ya mahojihano na Polisi na kupelekwa Dar kwa Mkurugenzi wa Upelelezi makosa ya Jinai kwa mahojiano.

Kwa mujibu wa Wakili wake, Jebra Kambole, amesema dhamana ya Nondo itatazamwa Jumatatu ijayo Machi 26, baada ya hakimu kuomba kusoma sheria inasemaje juu ya kuzuiwa dhamana kwake.

Imeelezwa kuwa, Nondo amesomewa mashtaka kwa makosa ya kutoa taarifa za uongo Mitandaoni na kosa la pili ni kudanganya kuwa alitekwa. Shauri limeahirishwa na mtuhumiwa amepelekwa rumande.

Leo Machi 21, 2018 Mwanasheria wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Paul Kisabo amewasilisha shauri la maombi Mahakama Kuu kutaka DPP, DCI, IGP wajibu mashtaka kwanini hawajampeleka Abdul Nondo Mahakamani na wamemshikiria kinyume na sheria mpaka sasa hivi.